Tuesday, November 13, 2012

HATU PASWI KUKATA TAMAA

Tunaishi kwenye jamii ya watu walio na mitazamo tofauti juu ya maisha,wana tenda matendo tofauti,wana fikiri kitofauti,hawafanani wanapo onyesha hisia zao juu ya masuala mbali mbali ya kimaisha.

kila mmoja ana mfumo wake wa maisha,na kila siku watu wanapoendelea na maisha,hukutana na changamoto mbali mbali za kimaisha.


Tumetofautiana jinsi tunavyokabiliana na kuta tua changamoto hizo,wapo wengine wanaokata tamaa ya maisha,kwa sababu ya matatizo yanayo wakumba.

Hakuna anayependa,kukumbwa na matatizo,ukiona huna matatizo mengi,mshukuru Mungu,ujue ni neema yake ipo juu yako.Ninacho amini ni kwamba “Hatu kuumbiwa kukata tamaa” ,lakini kuna watu tayari wameshakata tamaa na maisha,na hatuwezi kuwa acha waendelee na kukata tama,ungana nami katika kuihamasisha jamii yetu,ili tuone watu wakihamasika na kuyafurahia maisha.



Kama unajifunza kitu,na unahamasika,kupitia blog hii,ni andikie ujumbe kwenye e-mail yangu(baraka1990@gmail.com),maoni yako ni ya muhimu kwangu na nina yaitaji,ili niweze kuwa katika nafasi nzuri ya kuhamasisha jamii yetu.

0 maoni:

Post a Comment